Thursday, 28 May 2009

NI FC BARCELONA MSIMU WA 2008-09.

Dogo mwenye sifa ya uuaji wa kimya kimya anachezea mpira kama upo mkononi.



Raha ya sherehe msosi na raha ya ubingwa kombe.


Ahsante kocha kwa kile ulichotufundisha.


Dogo nimekukubalia umehitimisha shughuli.


Cha pili cha Lionel Messi.


Cha kwanza cha Samuel Eto'o.


Kweli soka shughuli kuna siku yaweza kuwa kwao na siku nyingine yaweza kuwa kwa mwenzako.


Yote maisha jamani mjipange upya msimu ujao.


Dogo jaribu tena haikuwa bahati yenu msimu huu.


Babu na wajukuu zake wakiwa na majonzi makubwa.


Mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona wamekamilisha azma yao ya kutwaa ubingwa wa soka wa barani Ulaya baada ya kuwashinda mabingwa wa soka nchini Uingereza Man utd.

Fc Barcelona ambao walikuwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa soka barani Ulaya, walifanikiwa kumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa na kufikia hatua ya kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Bao la kwanza la Barcelona lifungwa katika dakika ya 10 nma mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka nchini Cameroon Samuel Eto’o, huku bao la pili likifungwa na mshambuliaji chipukizi wa kimataifa kutoka nchini Argentina Lionel Mesi katika dakika ya 70.

Kufuatia hatua hiyo Barcelona wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya tatu katika historia yao toka klabu hiyo ilipoanzishwa mnamo November 29, 1899.

2 comments:

Anonymous said...

Kondo Manchester wamefulia

Anonymous said...

walishindwa kabisa kuonyesha ubabaishaji wao kweli wamefulia