Wednesday, 15 July 2009

BADO MWENYE NGUVU ATAENDELEA KUONGEZEWA.


Mubelwa Bandio. USA


Labda kwa jina lake wengi watasema HAPANA. Lakini kabla ya kujibu najiuliza ni nani aliyeita hilo tendo UBAYA. Unadhani wa upande mwingine hafaidiki?

Hebu angalia hilo lililopo nyuma yangu. UNADHANI LINA KAZI YOYOTE YA KUVUTIA? Lakini unadhani linagharimu kiasi gani kulitengeneza?

Inakadiriwa ni dola milioni 83 (mwaka 2006) na gharama zinaongezeka.

Unadhani ni watu wangapi wameshiriki kulibuni?

Unadhani ni watu wangapi wameshiriki kulitengeneza?

Unajua ni nchi ngapi zinashiriki kulitengeneza / kulitumia?

Angalia bendera hizo Unadhani katika nchi hizo ni wangapi wamepata ajira kutengeneza hilo?

Unajua linaendeshwa / kurushwa na maaskari ambao wana marupurupu kibao?

Unajua wengi wa wanaorusha hayo wanasomeshwa bure ili kutekeleza kazi yake?

Sasa hesabu wanaoshughulikia kusimamia "kazi" zake, wanaolifanyia matengenezo na ukarabati, wanaonufaika na mauzo ya mafuta na vipuri vyake na wengine.

Na hili ni moja kati ya "mitambo" mingi inayoendesha shughuli zake ulimwenguni.

Sote tunajua matokeo ya uwepo wa ndege za namna hii na athari zake ndizo tunazoweza kuita UBAYA. Lakini kwa yote niliyouliza na mengine mengi, bado swali linaendelea kuwepo kuwa KUNA FAIDA ZA UBAYA?

Hii ni kwa niaba ya Mubelwa Bandio. USA

No comments: