Hakuna ubishi kuwa kuna ngazi tatu za maisha ambazo ni Juu, Kati na Chini. Na katika ngazi hizo kila ngazi ina ngazi tatu yaani ngazi ya juu ina juu, kati na chini na ya kati vivyo hivyo na pia ya chini.
Hiyo inaweza kumaanisha kuwa aliye chini katika ngazi ya juu hana thamani (zaidi ya sifa) kuliko aliye juu katika ngazi ya kati.
Lakini bado kuna ukweli kuwa aliye chini katika ngazi ya juu ana heshima kuliko aliye juu katika ngazi ya kati japo mwenye heshima ana nafasi ndogo sana ya kutumia heshima hiyo kuinufaisha jamii.Swali:Kwani hujaona watangazaji wasio na majina kwenye redio kubwa wanapotoka na kwenda kuwa waelimishaji wakubwa kwenye redio ndogo?
Ama wasanii wasiowika kwenye vikundi vikubwa lakini wanaweza kuwa waelimishaji wakubwa na walio juu wanapokwenda kwenye vikundi vidogo?Labda!Walikuwa juu (kwenye sehemu zenye majina) na hawakuwa juu ya juu (maana hawakuwa na nafasi ya kuitumikia jamii huko) na sasa wameamua kushuka chini (kwenye sehemu zisizo na majina makubwa sana) na kuwa juu (kwa kuonesha uwezo na utumishi wao halisi).
Ama:Umesahau ulivyokuwa m'babe na mtemi wakati unamaliza darasa la saba (L.Y)na kisha ukaingia kidato cha kwanza ukawa "cha mtoto"?
Ndio!Kama wanasiasa wanaogombea urais kila uchaguzi na kushindwa wangeamua kugombea ubunge nina hakika kuwa wangepata, na hapo wangekuwa na nafasi na uwezo wa kuikosoa zaidi serikali kwa mamlaka na nguvu waliyonayo.
Wangeweza kuisahihisha serikali ndani ya mfumo halali na pengine kuongeza idadi ya wapinzani na kisha kuinyoosha serikali badala ya kumuacha Dr Slaa akiibana serikali peke yake (maana hata wenzake wengine wamefyata mkia).
Swali:Kwani Mrema, Lipumba, Mbowe, na wengine wangekuwa wabunge unadhani Bunge lingekuwa na ladha gani? Si hata wale wabunge "wafyata mkia" wangepata ujasiri wa kusema yale watakiwayo kuwasemea wananchi?Ninaloamaanisha:
Ni kuwa wanasiasa wetu wanapenda juu (urais) ambako hawako juu (hawaaminiki na hakuna dalili za wao kupata karibuni), basi wangeshuka chini (ubunge) wawe juu (wawe wengi, wenye nguvu na uwezo wa kuibadili serikali kama haitendi sahihi) na hapo tungeweza kuibadili nchi.Kumbuka kuwa huu ni mtazamo tu wa namna nionavyo tatizo. Labda nionavyo tatizo ndilo tatizo.
Naacha!Ila nawakumbusha wale "wapandao" kuwa wakiwa wanafikiria kuelekea juu basi wakumbuke usia wa Lucky Dube kuwa "be good to the people on your way up the ladder cause you'll need them on your way down" aliouimba kwenye chorus ya THE WAY IT IS.
HII NI KWA MUJIBU WA Mubelwa Bandio.
Saturday, 11 July 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Shukrani saana Mkuu kwa kushirikiana na WAUNGWANA katika kufikirishana hili. Tukumbuke kuwa "namna tuonavyo tatizo ndio tatizo" na kwa wengine kudhani "juu" ni kwema hata kama hakuwaweki "juu" ni namna wanavyoamua kile waonacho na kwa wengine ni tofauti.
Kila mtu anafanya maamuzi kutokana na namna aonavyo na twaona tofauti.
Blessings Man na PAMOJA DAIMA.
Post a Comment