BWM alianzisha MKURABITA na MKUKUTA vipi utekelezaji wake?
Mbona watanzania tuko vizuri kwenye makaratasi na maskini/wavivu field?
Kwa mfano Waziri wa Ardhi Nyumba na makazi wangeendeleza huu mpango.
Pia Maafisa mipango miji na Maafisa Ardhi wangegawa Ardhi au vipande vya ardhi kwa ajili ya watu wanaotaka kujenga makazi kwa bei nafuu.
Sasa hivi mtu akitaka kiwanja cha kujenga ardhi ni kama milioni 10 hadi 40 kulingana na ukubwa wa sehemu. Hizi ni bei za Arusha.
Dar bei ni rahisi kidogo kama millioni 2 hadi 10 hata hivyo mbezi ni ghali.
Sasa masikini watajenga kweli?
No comments:
Post a Comment