Kaka ki ukweli hakuna siku nzuri na njema kwa kila mwanaadamu hapa duniani kama siku yake ya kuzaliwa inapowadia.
Kaka hongera ninakupa, na hilo sitokuwa mchoyo kwako kwa sababu ni moja ya hatua ambayo imeipiga na pia wastahili kumshukuru mwenyezi mungu kwa kila jambo analokusaidia toka ulipoanza safari ya maisha mnamo august 10 mwaka fulani hivi huko nyuma.
Pia usimkufuru pale unapoona mambo yako yanakwenda kombo, katika imani ya dini yako inakufundisha kuwa hiyo huwa ni mitihani na kiimania mbayo huitoa yeye jalali.
Ninatambua mchango wako kwangu na wewe nadhani watambua mchango wangu kwako hivi ni rafiki wa kweli kwangu nami ni rafiki wa kweli kwao daina sitoacha kukupongeza pale unapokuwa na jambo jema, na utakapokuwa na jambo la uzuni sitochoka kukufariji.
Happy Birthday ndugu yangu.
Daima tutakuwa pamoja.
http://changamotoyetu.blogspot.com/
1 comment:
What can i say my Brother.
Nashukuru saaana na nitaendelea kusema kuwa UWEPO WAKO ni sehemu kuubwa saana ya maendeleo ya jamii na kwa kuunganisha nguvu zetu tutaweza kuifikisha jamii pale tunapopenda ifike.
Blessings
Post a Comment