Tuesday, 4 August 2009

JAMANI SALAMA SALAMA?

Wanajamii leo nimeona tujadili hili suala ambalo watu wengi sana mitaani wamekuwa wakiamini hivyo kuwa wawake wenye kipato kizuri ama wale walio na elimu nzuri, hasa wenye digrii ama zaidi ni vigumu sana kudumu katika ndoa ama mahusiano.


Na katika mahusiano yao huwa ni yenye migogoro mingi na mivutano sana kwa wenzi wao (Boyfriends ama Waumezao).


Humu jamvini wapo kidada wasomi wengi tu ambao wanaweza ”ku-share” uzoefu wao ama kutoa mtazamo wao katika hili. Kina Kaka pia mnaweza kutoa hoja na mitazamo yenu kuhusu hili kwani mahusiano yanahusu pande zote mbili


Ningependa watu tuchangie tukizingatia hasa maswali yafuatayo...


Je? unamaani kuwa huo mtazamo uliojengeka katika jamii una ukweli wowote?

Na kama ni kweli unafikiri nini hasa ndio chanzo?

Na kama unafikiri hii kitu haina ukweli wowote unafikiri ni kwanini basi kuna watu wanaona hivyo?

Mwisho toa ushauri wako kwa kidada wali kwenye kundi hilo ama kina Kaka walio nao katika mahusiano kuhakikisha mambo yanakwenda kama wengine tu.


NB: Kumbuka kuwa simaanishi wasichana wote walio katika kundi hilo bali ni walio wengi wao.






1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! Kwanza karibu saana maana tulikukosa jamvini.
Pili nirejee kwenye maswali. Ni kweli kuwa kuna huo "mjengeko" uliopo miongoni mwa baadhi ya wanajamii. Na kuna ukweli kuwa wanawake wamekuwa wakionekana kama kiungo dhaifu na watekelezaji wa matakwa ya wanaume na sababu kubwa ilikuwa ni support wanayopata toka kwa waume hao. Inapofikia mtu akawa na uwezo wa kujitegemea huwa hapendi kupelekeshwa kama ambavyo angepelekeshwa kama angekuwa na uhitaji. Hili ni kwa kila mtu na wakati mwingine maamuzi kama haya huwa hatuyaoni kwa kuwa anayeweza kuyatoa huamua kuepuka kujiingiza katika maisha yanayoweza kumfanya aonekane anatenda hilo. Mfano, mtu mwenye pesa za kuweza kumudu usafiri binafsi akiwa ndani ya daladala na likaonekana linachelewa kusubiri abiria watano milhali mtu huyo ana miadi mahala na anaweza kuchelewa, atakachofanya ni kushuka na kuchukua taxi. Lakini haya hatuyaoni kwa wingi kwa kuwa wenye uwezo wa kununua magari wananunua magari hayo hivyo hatuoni KIBURI chao kwenye daladala kwa kuwa hawapandi.
Kwa hiyo wanbawake wenye uwezo hawabadiliki, bali wanakuwa wanavyotakiwa kuwa ila sisi wenye mfumo unaoamini kuwa wanastahili kuwanyenyekea waume zao ndio tuonao tofauti yao.
Ndivyo ilivyo kwa jamii yoyote inayoaminika kuwa "minority" kuwa hata wanapofanya lililo la kawaida kwa wengine linapata "attention" ya kuvuka mipaka.
Ni hayo kwa sasa, wacha ni-pass mpira kwa wengine wacheze kivyao.
Blessings