Friday, 3 July 2009

KATU HAUTOSAHAULIKA.


Maandalizi ya mazishi ya Mfame huyo wa Pop yanatarajiwa kufanyika siku jumanne ya juma lijalo na yanatarajia kuvuta hisia za watu wengi kama ambavyo Michael Jackson mwenyewe alivyowahi kutabiri.


Zaidi ya watu milioni moja wanatarajia kuhudhuria misa ya mazishi hayo na kumuaga katika shughuli itakayofanytika katika uwanja wa mchezo wa kikapu wa Staples Center Arena uliopo jijini Los Angeles ambapo imekadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 750 watafuatilia mazishi yake kupitia runinga.

Familia ya Jackson imethibitisha kwamba yatakuwepo maonyesho kumuenzi nyota huyo wa muziki wa Pop mbele ya watazamaji wapatao 20,000 watakokuwa wameketi katika uwanja huo .

Inaaminika kwamba Rais Barack Obama alitumiwa mwaliko huku watu wengine maarufu watakaohudhuria ni Sir Paul McCartney mwimbaji Diana Ross aliyetajatwa katika mirathi ya mwanamuziki huyo na Liz Taylor ingawaje Quincy Jones amesema hatahudhuria kutokana na kukiri kwamba hawezi kuvumilia.

Hili ndilo Jeneza ambalo lina gaharama ya paund za kiingereza elfu 15.


Jackson anataraji kuzikwa katika sanduku lenye thamani ya paund elfu 15,000 litakalokuwa limenakshiwa na dhahabu yenye kipimo cha karati 14.

Jeneza hili ni sawa na lile alilozikwa nalo mwimbaji James Brown mwezi December mwaka 2006.

Pia mazishi hayo huenda yakavunja rekodi ya watu zaidi ya 75,000 watakaojipanga barabarani katika mitaa ya jiji la Memphis kumuaga mfalme huyo wa pop kushinda hata yale ya Princess Diana alietutoka miaka 12 iliyopita ambapo watu zaidi ya 250,000 walijipanga barabarani kumuaga.

Taarifa hii ni kwa hisani ya mdau mkubwa wa karibu Ibrahim Issa.



1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Naam. Ni ripoti kamili hii Kaka. Imepangiliwa vema na naamini itampa habari kamili kila asomaye.
Blessings Man