Tuesday, 16 June 2009

UNYENYEKEVU WENYE HESHMA.

Mmoja wa wachezaji wa timu ya Nyundo FC ya kisiwani Pemba akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Muungano, Muhammed Seif Khatib kwa unyenyekevu kabla ya mchezo wa hatua ya pili ya fainali ya michuano ya kombe la muungano Mufindi pamoja na Zanzibar uliochezwa kwenye uwanja wa Wambi mjini Mafinga mnamo June 13.


Katika mchezo huo timu ya Nyundo ilifungwa bao moja kwa sifuri na wapinzani wao FOYSA toka jijini Mbeya ambao walitawazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2009.


Katika mchezo wa hatua ya kwanza ya fainali uliochezwa Kisiwani Pemba kwenye uwanja wa Gombani timu ya FOYSA ilipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

No comments: