Tuesday, 7 July 2009

KUMBE JAMAA ALIKOSA USINGIZI SIKU CHACHE KABLA YA KIFO CHAKE.

MAZISHI ya mfalme wa Pop Michael Jackson yanatarajiwa kufanyika leo na baadhi ya watu mashuhuri ambao ni baadhi yao ni wasanii watakaokuwepo kumuaga mwanamuziki huyo mashuhuri ni pamoja na Kobe Bryant , Usher, Mariah Carey na wengine wengi wakiwemo mashabiki wa muziki wa aina mbalimbali.

Tamasha hilo la kumuaga Jackson litafanyika katika uwanja wa Staples Center jijini Los Angeles, California na mashabiki wasiokuwa na tiketi wameshauriwa kubaki majumbani mwao kushuhudia tukio hilo la kihistoria.


Mbali na waombolezaji kuwa na tiketi pia watatakiwa kuwa na ribbon mbili mkononi kabla ya kuingia katika uwanja huo.


Watu wengine mashuhuri Jennifer Hudson, Magic Johnson, Martin Luther King III, Lionel Richie na Stevie Wonder.


Send off hiyo pia itawashirikisha mamilioni ya mashabiki ambao tangu jana wamekuwa wakihangaika kupata tiketi ya kushiriki katika hafla hiyo .


Inatarabiriwa kwamba mitaa ya Los Angeles itakuwa na watu zaidi ya milioni 1.6 wakishiuhudia send off ya mfalme huyo wa Pop kupitia runinga zitakazokuwa zimewekwa katika mabarabara mbalimbali ya jiji hilo .


Baadhi ya vituo vya television vitakavyorusha matangazo hayo moja kwa moja ni pamoja na TV Guide Network, NBC, ABC, CNN, MSNBC na E ambapo watu bilioni moja wanatarajia kushuhudia tukio hilo kupitia runinga zao.