Saturday, 22 August 2009

Ahlan Wa Sahlan Ya Ramadhan!

Hakika ni nuru iliyotuwakia sote.



Ramadhani kareem ,Na Inshaallah tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kufunga swaumu zetu mwanzo wa mwezi huu mtukufu mpaka mwisho.




Tunamuomba Mwenyezi Mungu azipokee swaumu zetu na dua zetu kwa ujumla na atusamee dhambi zetu katika mfungo huu wa Ramadhani, nasi Waja wake tukumbuke kusali ama kuongeza ibada katika funga yetu.



Inshaallah Ramadhan Kareem.

3 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Ramadhani ikiwa njema kwa wale waitimizao (sote waIslamu, waKristo, waHindu, waYahudi na wengine) ina maana ULIMWENGU MZIMA UTAKUWA MWEMA. Tukizingatia yafundishwayo katika mwezi huu mtukufu (ambayo hayana mipaka ya kidini) tutatambua kuwa ndivyo tunavyotakiwa kuishi miaka yote na nyakati zote.
Kama ulimwengu ungeamua kuufanya mwezi huu uanzao sasa kuwa wa mabadiliko, ama kuamua kufanya haya mema yafundishwayo katika miezi mitukufu kama hii kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku, TUSINGELIA TULIAVYO KWA MATUSI, KEJELI, WIZI, UBAKAJI, UFISADI, MAUAJI, VITA, MATABAKA, MAKABILA, RUSHWA nk.
RAMADHANI NJEMA KWA ULIMWENGU MZIMA

Mzee wa Taratibu said...

Shukran mkuu nakutakia Ramadhani njema.

Yasinta Ngonyani said...

Nakutakia Ramadhani njema kakangu.