Thursday, 22 October 2009

TRA MPO AMA HAMPO? MNATAKIWA KUWEPO KAMA MPO?



Jamani ninaomba muelewe kwamba mimi si mnoko saaaaana ila ninataka niweke mambo sawa ili kila mtanzania aisha kwa fikra za maisha bora kwa kulinufaisha taifa na kujinufaisha mwenyewe pia.

Ninavyofahamu mimi ni kwamba kila anaefanya biashara ni lazima alipe kodi ambayo inasimamiwa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA ili kulinufaisha taifa katika kukuza uchumi na kupatikana kwa maendeleo ambayo tunayalilia kila siku.

Lakini pamoja na utaratibu huu ninaoujua mimi na watanzani wenzangu wanavyofahamu, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakienda kinyume na taratibu za kulipa kodi ili wafanye biashara zao kihalali pasipo kificho kwa kumuogopa filani bin fulani.

Huyu jaamaa unaemuona hapo juu, kamera ua PUNTERVERDE imemanasa mitaa fulani ya mjini Iringa akifanya biashara ambayo kwa hakika ninaweza kusema haina usalama wa kifya kwa asilimi chache sana na si dhani kama ni mnyama mbae tumekuwa tukimtafuna kila leo *NG’OMBE*.


1 comment:

viva afrika said...

toba yarabi..........isije kuwa nyama za watu hizi wajameni!!!!???