

Harusi ya kwanza ya wakenya wapenzi wa jinsia moja imefanyika mjini London Uingereza. Ndoa kati ya watu wa jinsia moja hairuhisiwi kwa mujibu wa sheria za Kenya, inaaminika ndiyo sababu watu wakaoana nje ya nchi.
Ni ndoa ya kwanza ya aina hiyo kufanyika hadharani kati ya wanaume wawili wanaotoka Afrika Mashariki, mjini London chini ya sheria iliyopitishwa mwaka 2005 nchini Uingereza ikiruhusu kutambulika kisheria uhusiano kati ya wapenzi wa jinsia moja.
Daniel Chege Gichia mwenye umri wa miaka 39 alimuoa Charles Ngengi mwenye umri wa miaka 40 aliyekuja London mahsusi kwa shughuli hiyo katika ukumbi wa Islington kaskazini mwa London.
Wengi wa wageni wa maharusi hao walikuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja au wanaotetea ndoa kama hizo pamoja na wale wasiobughudhiwa na uhusiano kama huo.
Wawili hao wanaotoka mkoa wa kati , wilaya ya Murang'a wanajiandaa kwenda Kenya kwa fungate yao baadaye mwezi .
2 comments:
tusijifanye hatuoni mambo wakati kwetu pia yapo, hebu tuzungumze jamani, tunaelekea wapi.
Lakini si ndo tabia mnazozitaka wasipochukuliwa hatua watu kama hawa,ndo maana taifa linapatwa laana za kila aina.Biblia inasema wamelaaniwa wafiraji sasa jifanyeni wajanja halafu Mungu akianza mambo yake mtasha na kumuuna vibaya.They look full of demons you can tell.
Post a Comment