Uongozi wa manispaa ya Iringa umewapongeza Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Tumaini cha mkoani humo kufuatia hatua yao ya kujitolea kufanya usafi kwenye maeneo ya stendi kuu.
Shukurani hizo zimetolewa na Meya wa manispaa Amani Mwamwindi kwa niaba ya viongzo wengine ambapo amesema kitendo cha wananfunzi hao kujitolea kufanya usafi ni sehemu ya kukamilisha jambo muhimu katika maisha ya kila ya mwanadamu.
Mwamwindi ambae alikuwa mgeni rasmi katika utaratibu huo wa usafishaji wa mazingira ya kituo cha mabasi cha mjini Iringa ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa uhifadhi wa mazingira kila mtu ana haki ya kuishi kwenye mazingira yaliyo safi na salama.
Amesema kuwa wanafunzi hao wa chuo cha Tumaini cha mkoani Iringa wametekeleza wajibu wao kwa kuifanya jamii kukaa katika sehemu zenye mazingira safi na salama ili kujiliwaza, kupata elimu, afya na kudumisha utamaduni wa usafi.
Nae, mmoja wa waratibu wa shughuli hiyo Nkirote Mwongera amesema lengo la shughuli hiyo ni kuwa karibu na jamii na kuihamasisha kutunza mazingira.
Amesema kilichofanyika ni moja ya malengo na kauli mbiu ya chuo ambayo inaelekeza kuhusu mafunzo, utafiti na huduma kwa jamii.
No comments:
Post a Comment