Saturday, 22 August 2009

Ahlan Wa Sahlan Ya Ramadhan!

Hakika ni nuru iliyotuwakia sote.



Ramadhani kareem ,Na Inshaallah tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kufunga swaumu zetu mwanzo wa mwezi huu mtukufu mpaka mwisho.




Tunamuomba Mwenyezi Mungu azipokee swaumu zetu na dua zetu kwa ujumla na atusamee dhambi zetu katika mfungo huu wa Ramadhani, nasi Waja wake tukumbuke kusali ama kuongeza ibada katika funga yetu.



Inshaallah Ramadhan Kareem.

Friday, 21 August 2009

ETI SI MWANAMKE !!!!!




Nyota wa riadha wa Afrika Kusini wa mbio za mita 800 za wanawake, kutokana na kuwa na misuli iliyojengeka kama mwanaume na uwezo wake mkubwa katika mbio hizo anafanyiwa uchunguzi wa jinsia yake kuthibitisha kuwa kweli ni mwanamke.


Semenya ambaye marafiki zake wanasema hajawahi kuwa na mpenzi wa kiume, ana misuli iliyojengeka, tumbo la miraba minne, sauti nzito kama ya kiume pamoja na vinyweleo usoni amekuwa akiandamwa na watu wanaohoji jinsia yake.


Kwa habari kamili unaweza ukawapa wadau link hii.

SEHEMU YA PILI YA SAFARI YA MTOTO WA MFALME WA DUBAI ALIPOTEMBELEA TZ.

Huyu ndie Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid al Maktoum mtoto wa mfalme Mohammed bin Rashid Al Maktoum wa Dubai.


Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid al Maktoum safari yake ilikuwa ndefu sana na zipo picha nyingine nyingi alizopiga akiwa katika moja ya mbuga za wanyama hapa nchini Tanzania.

Hii ni sehemu ya pili ya safari hiyo.

Sehemu ya tatu endelea kutembelea blog hii.

Thursday, 20 August 2009

WASWAHILI WANASEMBA NGOMA BADO MBICHI.


Mahakama ya rufaa nchini imethibitisha kupokea rufaa iliyowasilishwa na serikali dhidi ya kupinga uamuzi wa mahakama kuu wa kuwaachia huru washtakiwa tisa wa kesi wa mauaji ya wafanya biashara watatu na dereva teski mmoja mnamo mwezi Januari mwaka 2006.


Msajili wa mahakama ya rufani nchini Francis Mutungi ameyasema hayo jijini Dar es salaam kuwa rufani hiyo namba 254 ya mwaka 2009 imeshapokelewa na kinachoendelea hivi sasa ni hatua za kuchukuliwa kwa kumbu kumbu za kesi husika kutoka mahakam kuu ya Tanzania iliyoanza mwezi septemba mwaka 2006.


Mutungi amesema katika rufani hiyo serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekata rufaa dhidi ya Zombe na wenzake walioachiwa huru mwanzoni mwa juma hili.


Mapema katika Notis yake ya serikali aliieleza kuwa ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo dhidi ya Abdallah Zombe na wenzake wanane ulikuwa unatosheleza kwa watu hao kutiwa hatiani.


Wednesday, 19 August 2009

HAKIKA WASTAHILI PONGEZI KAKA.


Hongera sana kaka kwa kufikia hatua hiyo, Naomba nikumbushe hivi ni mishumaa mingapi unaizima leo?



Zawadi zako ziko pale pale zinakusubiri mdau.



HAPPY BIRTHDAY AGAPE MWANA WA MSUMARI TOKA USAMBAANI, LUSHOTO TANGA.

BADO MBICHI.


SERIKALI imesema haijaridhika na hukumu iliyowaweka huru watuhumiwa kwenye kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva mmoja na imeamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.


Katika hukumu iliyosomwa na Jaji Salum Massati juzi, haikuweza kuithibitishia mahakama kuwa watuhumiwa hao tisa, akiwemo mkuu wa zamani wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe, walishiriki katika mauaji hayo na kwamba waendesha mashtaka walishindwa kuwafikisha mahakamani wauaji na hivyo kuagiza wasakwe.


Kaimu Mkurugenzi wa Mashtaka, Mary Lyimo alisema katika taarifa yake jana kuwa, ofisi yake imeamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo ambayo pia imepokewa kwa hisia tofauti na wananchi.


"Katika uamuzi huo, Mahakama Kuu ya Tanzania, baada ya kuuchambua ushahidi uliotolewa na misimamo mbalimbali ya kisheria, iliona kuwa upande wa mashtaka (Jamhuri) ulikuwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka yake dhidi ya washtakiwa pasipo kivuli cha mashaka kama inavyotakiwa katika mashauri ya jinai," inasema taarifa yake.


"Hivyo iliamua kuwaachia huru washtakiwa wote waliokuwepo. Uamuzi huo umepokewa kwa hisia tofauti na umma. Ofisi hii inapenda kuufahamisha umma na kuuhakikishia kuwa hatukuridhishwa na uamuzi huo; hivyo sasa tunaanza mchakato wa kukata rufaa kwa kutoa Taarifa ya Nia ya Kukata Rufaa."


Upande wa mashtaka ulionekana kuyumba wakati wa majumuisho yake wakati ulipomwomba jaji kuwatia hatiani watuhumiwa na kwamba kama aliyekuwa mshtakiwa asingepatikana na hatia ya kuua bila ya kukusudia, atiwe hatiani kwa kushiriki kosa baada ya kosa, ombi ambalo Jaji Massati alilikataa kwa maelezo kuwa halimo kwenye mashtaka.


Wakati serikali ikijipanga kukata rufaa, wanasheria mbalimbali wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya hukumu hiyo, wakiwemo ambao walisema kutotiwa hatiani kwa washtakiwa hao, ambao wote walikuwa askari wa Jeshi la Polisi, kumetokana na uzembe wa serikali katika kufanya uchunguzi na kuandaa mashtaka.


Naye wakili wa kujitegemea na mtaalamu wa masuala ya sheria, Profesa Abdallah Safari amesema kushindwa kwa serikali katika kesi hiyo ni kashfa.


Profesa Safari aliiambia Mwananchi kuwa, kuachiwa huru kwa watuhumiwa hao kunaonyesha kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa ya kisheria katika pande zote zilizohusika na kesi hiyo.

Profesa Safari alisema inawezewekana Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa wakati huo aliamua kufungua kesi hiyo kwa kuzingatia taarifa ya tume ya Jaji Musa Kipenka kutokana na joto la shinikizo la kisiasa kwa wakati huo.


“Unajua tume hii iliundwa na Rais Kikwete... inawezekana DPP aliamua kuichukua taarifa hiyo kama ilivyo na kufungua kesi bila kuangalia zaidi mbinu za kisheria, alisema Safari.


“Siku zote lazima ieleweke kuwa duniani kote kesi haiendeshwi kisiasa, bali inaendeshwa na ushahidi uliopo,” alisema Profesa Safari ambaye aliwahi kugombea uenyekiti wa chama cha kisiasa cha CUF.


Mwanasheria huyo alisema Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ndiye aliyekuwa na wajibu wa kuwakamata wauaji na kuwasilisha faili lao kwa DPP.


“Sijaziona nyaraka kutoka kwa DCI kwenda kwa DPP, lakini nahisi upelelezi haukufanywa vizuri,” alisema Profesa Safari na kuongeza kuwa serikali haikupaswa kushindwa katika kesi hiyo kwa kuwa ilikuwa na kila kitu.


“Hii ni sawa na mpishi kuwa na kila kitu, lakini ameshindwa kupika chakula kizuri, hivyo kuna umuhimu serikali ikajiangalia vizuri katika hili.”


Aliitaka serikali kutokata rufaa kwa jazba na badala yake ijiridhishe na ikiwezekana ijaribu kuomba msaada kutoka kwa wanasheria wengine wa kijitegemea wenye uwezo wa kupambana na kesi za namna hiyo.


Msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kennedy Gaston alisema: “Zombe alisema kulikuwa na majibizano ya risasi; alikataza miili ya marehemu kuchunguzwa huku akitaka izikwe mapema. Haya yote ni makosa ambayo yangeweza kumtia hatiani.


Si lazima kukimbilia kosa moja la mauaji.”


Msomi mwingine wa UDSM, Lucy Eusebio alisema: “Katika kesi ya mauaji kuna mambo mawili, kuachiwa huru au kunyongwa hadi kufa, na kuna kanuni ya sheria inayosema ni heri kuwaachia wahalifu 100 kuliko kumfunga mmoja asiye na hatia.


“Kwa maana hiyo katika kesi ya mauaji inatakiwa ushahidi ujitosheleze kwa asilimia 100. Hata kama kutakuwa na asilimia 99 ya ushaidi unaoonyesha kuwa mtuhumiwa aliua, hiyo asilimia moja iliyopungua itaifanya mahakama impendelee mtuhumiwa.”


Wakili wa kujitegemea Anney Semu, alisema Jaji Massati ametoa hukumu hiyo kwa haki kwa sababu amefuata sheria na taratibu za kimahakama.


"Ila waendesha mashtaka walishindwa kuendesha kesi hiyo inavyopaswa kutokana na kwamba walikuwa wakisukumwa na hisia za wananchi ya kwamba Zombe ndiye aliyeua," alisema Semu na kueleza udhaifu wao kuwa ni kushindwa kuwachambua washtakiwa na kuwahusisha ipasavyo na mauaji hayo.


"Walichochanganya ni kushindwa kufuatilia kosa lilikuwa linasemaje, badala yake wakafuata hisia zilizochochewa na wananchi kuwa Zombe ndiye aliyeua."


Naye Profesa Issa Shivji alisema, hukumu hiyo imetokana na jaji huyo kutumia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.


"Majaji kazi yao ni kusikiliza ushahidi wa pande zote unaotolewa.


kiwa ushahidi huo utaletwa kinyume, hukumu yake inaweza kuwa tofauti na kosa lenyewe," alisema Profesa Shivji.


Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo waendesha mashtaka wanapaswa kuwa makini ili kutoa ushahidi ambao unaendana na kosa lenyewe.


Wakati huo huo, Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limeanza kujipanga upya kumtafuta polisi alinayedaiwa kutekeleza mauaji hayo yaliyofanywa mwaka 2006, Koplo Saad Alawi, ambaye alitoroka muda mfupi baada ya mauaji hayo.


Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova aliliambia gazeti hili jana kuwa, kazi ya kumtafuta mtuhumiwa huyo ilianza mara moja baada ya hukumu hiyo.


“Tumeanza mkakati wa kumtafuta mtuhumiwa huyo kama mahakama ilivyotuagiza.

Tutajitahidi kumsaka mahali popote mpaka atakapopatikana,” alisema Kova, ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa kamanda wa polisi mkoani Mbeya.


“Tunaheshimu agizo la mahakama, ndiyo maana tunaahidi kumtafuta ndani na nje ya nchi. Licha ya kwamba mtuhumiwa alikuwa akitafutwa tangu awali, kwa agizo hili tunaongeza nguvu zaidi,” alisema Kova.


Kova alisema moja ya mbinu itakayotumia kumsaka mtuhumiwa huyo ni kuiomba jamii ishiriki katika kutoa taarifa za mahali alipo.


“Sikiliza... jeshi hili halijawahi kushindwa kumnasa mtuhumiwa na wale wanaotafutwa muda mrefu ndiyo tunawapata kirahisi, hivyo nina hakika tutampata,” aliongeza.


Akizungumzia askari ambao walifukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji hayo, Kamanda Kova alisema polisi inaandaa utaratibu maalumu utakaotangazwa na makao makuu hivi karibuni.


Habari zinasema kuwa baadhi ya watuhumiwa walioachiwa huru wakati kesi hiyo ikiendelea, walikuwa wakilipwa nusu mshahara na sasa wamerejeshwa kazini.

Tuesday, 18 August 2009

HIVI UNAFAHAMU MTOTO WA MFALME WA DUBAI ALIZULU TANZANIA?

Huyu ndie Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid al Maktoum mtoto wa mfalme Mohammed bin Rashid Al Maktoum wa Dubai.



Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid al Maktoum safari yake ilikuwa ndufu sana na zipo picha nyingine nyingi alizopiga akiwa katika moja ya mbuga za wanyama hapa nchini Tanzania.
Hii ni sehemu ya kwanza ya safari hiyo.
Sehemu ya pili endelea kutembelea blog hii.


Monday, 17 August 2009

ZOMBE YU HURU.


Mahamaka kuu jijini Dar es Salaam imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar es Salaam Abdallah Zombe na wenzake baada ya kukutwa hawana hatia ya kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara ya madini.



Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Kiongozi Salum Massati baada ya mahakama hiyo kuchambua ushahidi wa upande mashtaka na ule wa utetezi uliokuwa na mashahidi 37.



Alipozungumza nami kwa njia ya simu wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwepo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo ikitolewa.



Amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo haumuoneshi mshitakiwa hata mmoja kuwa anahusika na mauaji hayo badala yake unamtaja mtuhumiwa mwingine anayetajwa kwa jina la koplo Sadi.



Amesema ushahidi huo unawaunganisha washitakiwa walioachiwa huru jioni ya leo,lakini kwa kuzingatia kuwa mtu anyesadikika kuwa anahusika na mauaji hayo hakuwepo mahakamani kwa hivyo washitakiwa waliosalia hawawezi kupatikana na hatia.



Hata hivyo mpaka hukumu hiyo inatolewa haikuweza kufahamika mahali alipo Koplo Sadi lakini mashahidi wote na baadhi washitakiwa walionesha kuwa walikwenda katika eneo la msitu wa pande uliopo mbezi Luis jijini Dare s salaam ambapo wanamtaja koplo Sadi kuhusika na mauaji hayo.



Taarifa kutoka mahakamani hapo zimeleeza kuwa kesi hiyo imehudhuriwa na umati mkubwa wa watu hali ambayo imeifanya mahakama hiyo kuamuru baadhi ya watu kutoka nje na kusikiliza kesi hiyo kupitia vipaza sauti.



Mkuu huyo wa zamani wa upelelezi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam na wenzake walikuwa wanatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge Mkoani Morogoro na dereva taxi mnamo January 14 mwaka 2006 kwenye msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis jijini Dar es salaam.Kesi hiyo ilianza mwaka 2006 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, kesi hiyo ilihamishiwa mahakama kuu.




MOTO WATEKETEZA GHALA YA MURZAH OIL.

Moshi ukifuka kwa nje.
Moto ukiteketeza sehemu ya ghala la kuhifadhia rola za karatasi za kutengenezea maboxi katika kiwanda cha Jumbo Packaging Print company’ ambacho ni mali ya MURZAH OIL kilichopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam.

Wafanyakazi wakijaribu kuokoa baadhi ya mali.


Wafanyakazi wakijaribu kuokoa baadhi ya mali.


Mwenyekiti wa Kampuni hizo za Muzarh Bwana Zakaria Abdul.



Sunday, 16 August 2009

NIMETUMWA KWENU NAMI NAWAKILISHA.


Napenda kutanguliza shukrani za dhati kwa yale yote mnayo changia kuhusu maendeleo ya taifa na kushauri jamii pale inapokosea.

Ningependa nianze kama ifuatavo,mimi ni mwanamke mwenye umri wa kiaka 29 ninafanya kazi katika kampuni moja hapa Tz.

Miaka minne iliyopita niilibahatika kupata rafiki wa kiume ambaye tulikuwa tunasoma wote chuoni, alinipropose kuwa ananipenda na yupo tayari kunioa wala cyo kwa kunichezea nilikubali tukawa ni marafiki wa uchumba na tutakuwa tunaishi kama mke na mume tunashirikiana kwa kila kitu.

Wazazi wake /kaka/dada walikuwa wanafaham hilo kuwa mdogo wao anamchumba wapo wote ,niilibahatika kumuona mama yake /mama mkwe mtarajiwa tukiwa chuoni mara mbili tuuu, tena alikuwa akipita naambiwa nimpelekee maziwa huwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Tuliendelea na urafiki wetu hadi tulipo maliza chuo nilikuwa ninaujauzito wake tayari na tulikuwa tunasubiri kuitwa kwa kazi kwa sababu tulifanya na interview mapema tukiwa chuoni bado.

Nilimwambia kuwa mimi nimmjamzito akakubali na akanambia nikawaambie home ili tufanye maandalizi ya harusi.

Hapo ilikuwa ni mwaka 2007, niliwaambia home kama ujuavo wazazi walikasirika sana kiac kwamba mdingi alipata na Presha kwa kuwa hakutarajia kitu kama hicho ukizingatia mimi ni first born wake, mama alim please hadi akatulia but alisema okay fine, kama ameamua basi sawa tumwachie afanye atakavo koz yeye siyo mtoto mdogo tena.

Mie nikamwambia mwenzangu kuwa nimesha waambia home ila kwakuwa nimepata ujauzito nikiwa nje ya ndoa unatakiwa kuja home ujitambulishe na vilevile kuomba msamaha ili ijulikane utaoa au vipi.?

Heeeeeee utafikiri nilichokoza nyuki kipindi hicho ndo alikuwa anahangaikia maswala ya kazi akanambia ati hawezi kuja home saivi kwa vile anahangaikia maisha kwanza, nikamwambia wazazi wangu wanataka wakuone na pia wajue utalea mimba au utakataaaaa, basi tokea hapo hatukuonana tena tangu aniache chuoni mimba ni changa hadi akapata kazi nikamkumbusha tena lakini ndo alikuwa hataki hata kusikia akaanzisha Jingine la kuwa ngoja nijipange vizuri kimaisha hapo mie tumbo linazidi kukua kila siku.

Mungu si Athuman nilipata kazi kama mhasibu , niliweza kujikimu kwa vitu vidogovidogo, yeye nilikuwa nikimwammbia nina shida na hela ananiambia hana, na wakati huo alikuwa kabadilika sana hata kuniona saa zingine inakuwa kama ni karaha vile, mi kashukuru mungu kuwa nina kazi basi nitaishi kwasababu kama ni maisha nilimsaidia kwa kila kitu wakati tupo chuoni hadi anapata kazi ni juhudi zangu pia nilichangia lakini nilipo enda kwake ikawa ni shida tupu.

Tuliendelea na maisha ya aina ile hadi nilipojifungua home, kumbuka hadi naenda home kujifungua alikuwa bado hajaenda kuwaona tena wazazi ingawa ndo aliyekuwa wa kwanza kunilazimisha kuwaambia kuwa mi ni mjamzito,.

Nashukuru mungu nilijifungua salama mtoto wa kike, yupo hadi sasa lakini siku ambayo naenda kujifungua aliniachia hela ambayo niitumia kwa tax tuuu ,yeye kama yeye alisema mshahara haujatoka bado mi nikasema fine hakuna shida madam nina pesa inaingia bank na mimi na pia WAZAZI wangu walinihudumia kwa kila kitu sikuona shida yoyote ile, siku niliyo toka hospital alikuja kumuona mtoto na kuanza kumkagua kama anafanana na yeye au vipi nikamwacha akamwangalia then akaniaga kuwa atasafiri kurudi kazini, hela hana ila atanitumia akifika.

Nikasema sawa, ndugu yangu tangu alivo ondoka hakurudi tena wala kutuma hela ya matumizi ya mtoto hadi nikarudi kazini baada ya likizo ya uzazi kuisha.

Chakushangaza nilipofika alishangaa sana kwa sababu sikumtaarifu kama nitarudi lini.

Wazazi wangu walikasirika sana, kwamba wamemtunzia mimba, kwa kweli hata miye nilijisikia vibaya koz huwez amini hata mama yake hakuwahi kunijulia hali katika kipindi chote kile alikuwa anakuja kuwasalimia ndugu zake hapo anapo fika yeye ni kilometa 90 kufika kwangu lakini hajawah kuja hadi kesho ninavo ongea.

Sasa ishu inakuja kwamba huyu niliye zaa naye ilifikia mahali nilichoka kumvumilia kwa sababu alianza tabia za ajabu alishakuwa na mwanamke mwingine tena, nikamwambia mimi na yeye basi kwanza sijaona chochote kile alichonisaidia kwa mtoto hadi kumpigia kelele sana.

Wazazi wangu wamenambia kuwa hawataki kumuona na kusikia kuwa anataka kunioa kwa sababu mpaka sasa mtoto kesha kuwa anakaribia miaka miwili sasa, pia kwa sasa tangu mwezi wa pili amekuwa kunisumbua sana kuwa anataka kunioa ikafikia mahali alitaka kujiua lakini mi namwambia kuwa sipo tayari nishaamua kuishi pekeyangu tuuu.

Kwani nikiishi mwenyewe ni makosaaa?????? ametangaza mitaani kuwa mimi ni mkewe ili hali hatujafunga ndoa bado je hilo pia ni sawaaaaaa???

NDUGU ZANGU NAOMBENI USHAURI KWA HILI KWANI MIM IHAPA NISHAMWAMBIA KUWA SITAKI TENA KUOLEWA NA YEYE ,AKAOE MTU MWINGINE KWASABABU HAKUNA NDUGU YAKE HATA MMOJA AMBAYE ALISHA MUONA MTOTO ZAIDI YAKE YEYE BABA WA MTOTO TUUUU.

NAOMBA USHAURI KWA HILI........niishi kwa amani


THE NGOMA AFRICA BAND AKA FFU KUWASHA MOTO MWINGINE AUGUST 21-09.








The Ngoma Africa Band watawasha moto mwingine katika onyesho la wazi Alafia-Afrika Festival 21-08-2009 Mjini Hamburg,Ujerumani

PIA Balingen Festival, 22-08-2009 mjini Balingen, Ujerumani.

Bendi maarufu ya mziki wa dansi The Ngoma Africa band inatarajiwa kupanda jukwaani siku ya ijumaa 21-08-2009 katika onyesho kubwa la wazi Alafia-Afrika Festival litakalo fanyika mjini Hamburg, katika ya mji sehemu maarufu ya Hamburg-Altona,Kamanda Ras Makunja atakiongoza jukwaani kikosi chake The Ngoma Africa Band aka FFU kuwapa burudani ya kufa mtu washabiki katika onyesho hilo litakalo fanyika majira ya jioni kuanzia saa 1.00 hadi Saa 3 .00 Usiku Ngoma Africa wakakuwa jukwaani,wakiwajibika.

Baada ya Hapo karandinga la bendi hilo litatumua vumbi kuelekea mjini Balingen, ambako bendi hiyo itatumbuiza katika onyesho lingine kubwa la wazi Balingen Afrika ! Festival siku ya Jumamosi 22-08-2009,ambako washabiki wanaisubiri kwa udi na uvumba bendi hiyo.#
Wasikilize mziki wao hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica

Saturday, 15 August 2009

KUIGA TUNAKOIGA, TWAIGA NA VYA KIJINGA?


Vipo vingi vya kuiga, vinavyopaswa kuigwa,


Hivyo mtu akiiga, hata yeye ataigwa,


Ubaya siyo kuiga, ni vile vinavyoigwa,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?





Mashindano ya urembo, tumeiga asilani,


Wanatao kwa mapambo, wandele majukwaani,


Wanasa kama urimbo, na nusu nguo mwilini,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?





Hilo tumelikubali, tukasema ni modeni,


Vichupi na suluali, na mavazi ya fukweni,


Wakiyajibu maswali, kwa lafudhi za kigeni,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?





Twashindanisha watoto, kwenye urembo jamani,


Urembo huo ni ndoto, kwa watoto wa shuleni,


Watoto wawe watoto, twadhulumu jamani,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?





Hebu pita kijiweni, mwangalie Solomoni,


Suruali matakoni, na kofia kisogoni,


Aimba Kimarekani, kakulia Kiwalani,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?





Tunaporudi nyumbani, twatoka ughaibuni,


Twajifanya ni wageni, tumesahau kingoni,


Ndoo ya maji bafuni, twataka ya mvua jamani,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?





Tuige vilivyo bora, vyenye tunu na thamani,


Tusiwe tunajichora, kwa kuiga vya kihuni,


Tuige bila papara, vya kutupa ahueni,


Kuiga tunakoiga, twaiga na vya kijinga?




ENZI ZA MWAAAALIMU!!!!!!!!!


Thursday, 13 August 2009

KWELI BONGO TAMBARALE.



Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.


Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.


Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.


Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.


Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :


Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk).


Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.


Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda;




Zingatia tarehe za kujiandikisha.


Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano.
UMOJA NI NGUVU!

Wednesday, 12 August 2009

BAN KI –MOON AFUNGUA KONGAMANO LA MAZINGIRA


Dunia inaweza kukabiliana na Matatizo yanayoikumba kama vile umaskini katika nchi zinazoendelea, njaa na magonjwa bila kuharibu Mazingira.

Hayo yameelezwa leo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wakati akifungua kongamano la kimataifa la mazingira Nchini Korea ya Kusini.

Ban Ki-Moon ameeleza kuwa uharibifu wa mazingira unapelekea Upungufu wa Maji ambao unaathiri idadi kubwa ya watu na kuleta madhara ya magonjwa kama vile utapiamlo.

Pamoja na kuipongeza Korea ya Kusini kwa kuwa Mfano bora kwa utunzaji wa mazingira, ameiasa pia kuongeza jitihada zaidi katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, aliongea kwa kusema kuwa nguvu za pamoja zinahitajika kutoka katika sekta zote za jamii, ili kukabiliana na suala zima la uharibifu wa Mazingira.

Ban Ki-Moon alisisitiza kuwa , Nchi zinazoendelea ni lazima ziwe na mipango na matendo ambayo ni lazima yapimike na kuripotiwa ili kufikia malengo ya kukabiliana na suala zima la uharibifu wa Mazingira.

Kongamano hilo la siki mbili la Mazingira litajadili pia suala la sera mchanganyiko zitakazoweza kutumika kushughulikia suala zima la matumizi ya Nishati na usimamizi wa mazingira kwa ujumla.

Kongamano hilo linahururiwa na wataalam mbali mbali wa masuala ya mazingira na Mawaziri wa Mazingira kutoka nchi mbali mbali Duniani ikiwemo Tanzania.

MAKUMBUSHO YA CHIEF MKWAWA.

Sehemu ya makumbusho ya shujaa Mkawa.

Monday, 10 August 2009

HAPPY BIRTHDAY MUBELWA BANDIO.


Kaka ki ukweli hakuna siku nzuri na njema kwa kila mwanaadamu hapa duniani kama siku yake ya kuzaliwa inapowadia.


Kaka hongera ninakupa, na hilo sitokuwa mchoyo kwako kwa sababu ni moja ya hatua ambayo imeipiga na pia wastahili kumshukuru mwenyezi mungu kwa kila jambo analokusaidia toka ulipoanza safari ya maisha mnamo august 10 mwaka fulani hivi huko nyuma.


Pia usimkufuru pale unapoona mambo yako yanakwenda kombo, katika imani ya dini yako inakufundisha kuwa hiyo huwa ni mitihani na kiimania mbayo huitoa yeye jalali.


Ninatambua mchango wako kwangu na wewe nadhani watambua mchango wangu kwako hivi ni rafiki wa kweli kwangu nami ni rafiki wa kweli kwao daina sitoacha kukupongeza pale unapokuwa na jambo jema, na utakapokuwa na jambo la uzuni sitochoka kukufariji.


Happy Birthday ndugu yangu.


Daima tutakuwa pamoja.

http://changamotoyetu.blogspot.com/



Sunday, 9 August 2009

NDUGU ZETU WANAANGAMIA.


Moja ya magonjwa yanaindama jamii ya Malaysia ni Cancer inayosababishwa na uvutaji wa sigara, kwa mujibu wa Takwimu za wizara ya Afya hapa 7 kati ya vijana 10 wanavuta sigara na takwimu pia zinasema wengi wa hawa vijana wanaanza kuvuta sigara katika umri wa miaka 15 hadi 18 ambapo baada ya kufika miaka 26 wanakuwa wamekubuhu.



Pia takwimu zinasema 4 kati ya vijana wa kike kati ya umri wa miaka 17 na 30 wanavuta sigara kwa Malaysia.


Hivyo serikali kupitia wizara ya afya inaendesha kampeni kwenye magazeti na kupunguza maeneo ya kuvutia sigara na kuweka sheria kali kwa wanaokiuka ikiwa ni pamoja na hairuhusiwi kuvuta sigara kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu, Majumba ya Sinema, Migahawa ya chakula, Kumbi za sinema, Mall, Sokoni na kila sehemu ya mikusanyiko mingi ya watu na kutaka kila kumbi za burudani kuwa na mahala maalum kwa wavuta sigara.


Naimani sisi wanablog tunaweza kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi kwani vijana wengi wanatembelea kwenye blog zetu, Wavutaji bongo mpoo!!

ULIWAHI KUISIKIA HII?

Kulikuwa na njemba moja imeowa ,tatizo la njemba huyo ni kukojoa kitandani kila siku ,hatimae mke ustaarabu na uvumilivu ukamshinda ,na siku moja akaamua kumkoromea mumewe kuwa ,kazi ya kufua mashuka na kuanika godoro kila siku itamshinda na anaona aibu maana majirabu wameanza kuhoji mbona kila siku kunafuliwa mashuka na kama haitoshi hata yeye mikono imeanza kuota masuguru na kuchunika kwa tindikali ya kojo lake.

Sasa akamuweka kiti moto mumewe na kumwambia kuwa leo ni siku ya mwisho na ikiwa usiku wa leo atakojoa kitandani basi itakuwa ndio mwisho wa wao kuwa mke na mume kila mtu atashika njia yake na kwa ufupi ndio atakuwa ameachika.

Kwa kweli siku ile njema yule alipata mtihani mkubwa sana na aliona hatima ya ndoa yao inafikia mwisho au ipo ukingoni kabisa.

Kwa bahati usingizi ukawachukua ilipofika alfajiri ,yule mke kitu cha kwanza alianza kupapasa kuona kama kuna kojo limetapakaa kwenye kitanda ,hakuona kitu na kufikiri kuwa mkwala aliomchimbia mumewe umefanya kazi ,dah kuja kutahamaki anasikia harufu ya kinyesi na kuona kila kukicha ile harufu inazidi kunukia ndani ya chumba chao ,kutahamaki kumbe mumewe siku ile hakukojoa amekunya.

Yule mke akili ikamzunguluka na kuona ya leo ni mpya tena ya aina yake ,ikabidi atulie na kumwita mumewe kwa upole kabisa kabisa huku akionekana mwenye kumshangaa na siejua la kufanya ,haya mume wangu embu nieleze hii ya leo ni ipi maana mtu mzima wewe sasa unaniletea miujiza ?

Yule njemba akamwambia mkewe ,kwanza akataka msamaha na kumwambia kila alalapo inapofika usiku wa manane humjia mtu usingizini na kumuamrisha akojoe kitandani au sivyo atamuua ,ila usiku wa kuamkia leo alipokuja kuja nikampa ile issue na mkataba wako ,hata hivyo haikuwa salama akaniamrisha nifanye kitendo mbadala ,ninye au sivyo atanitoa roho ,nikaona bora ya hivyo kuliko kutolewa roho ,nisamehe mke wangu sio lengo langu ila ni maswaibu ambayo yapo nje ya uwezo wangu ,yule mke kusikia hivyo aliangua kilio haijulikani kwa nini.

Saturday, 8 August 2009

MANENO MBOFU MBOFU.


Nilipokuwa ninaendelea kukuwa niliambiwa na wakubwa zangu waliokuwa mbele kiumri kwamba mtu anaechezea kimvuli chake huenda akapata matatizo! hivi ni kweli?



Nisaidieni janani hili ni la kweli?

ISIMILA STONE AGE.


Sehemu ya Isimila Stone Age iliopo mkoani Iringa na mara kadhaa imekuwa ikitembelewa na wageni kutoka nchi mbali mbali.

Thursday, 6 August 2009